Ukiongelea kampuni nguli na mkongwe kwenye ruti ya DAR-MWANZA, huwezi
ukamuacha Zuberi & Sons, kampuni hii imedumu miaka nenda rudi
tangia kipindi kile cha Gonga shimo (Rough Road).
Enzi hizo Ukitoka Mwanza saa 12 asubuhi singida unafika saa 11 jioni,...
Kampuni
hii imekua ikichepua kila siku wakianza na Masufuria(Local made bus)
mpaka Andare na Volvo Bus. Baada ya kusoma upepo wa kibiashara Mzee
Zuberi aliuza baadhi ya mabasi na kuhamia kwa mabasi ya kichina ili
kwenda na wakati na soko la mabasi.
Kadri kampuni ilivyokuwa inakuwa kubwa, zikazaliwa kampuni nyingine pia kutoka Zuberi, ambazo ni Kisesa na Zube.
Kwa kwenda na TREND ya soko kampuni hii inamiliki basi kadha wa kadha za kichina ikiwa ni Higer na ZhongThong.
Kudhihirisha
unguli wake wa kibiashara kampuni hutoa gari tano mpaka sita kwa ruti
ya Dar - Mwanza ikiwa ni Mchanganyiko Zuberi na Kisesa.
No comments:
Post a Comment