BREAKING NEWS

Basi la kampuni ya Safari  njema Leo mchana 30/10/2016 , limepata ajali maeneo ya kimara stop over. Ajali hio imehusisha lori la lilobeba sement na basi la safar njema lililokuwa likitokea Dodoma kueleke Dar.

Basi pamoja na lori hilo yameteketea kwa moto uliolipuka baada ya lori kuligonga basi .Mpaka tunaleta taarifa hii. habari zisizothibitishwa zinasema aliefariki ni mmoja na kuacha majeruhi 16.



 





Basi la Kampuni ya Hood Limited linalofanya safari zake kati ya mbeya na Arusha leo saa 8 (27/10/2016)Mchana limepata ajali maeneo ya mlima Kitonga mkoani Iringa.

Chanzo cha ajali ni kufeli kwa mfumo wa upepo wa breki na kugongana uso kwa uso na lori la mafuta hivyo kusababisha basi kupinduka.

Hadi tunapata habari ajali hii imegharimu maisha ya abiria mmoja (1) na Majeruhi 43. waliofikishwa hospitali ya Ilula na Hospital ya mkoa wa Iringa.








Basi la kampuni ya Hood T...AXV linalofanya safari zake kati ya Arusha na Iringa, limepata ajali jana mjini Arusha, baada ya kufeli breki katika makutano ya barabara na kuparamia baa iliokuwa jirani.

Ajali imetokea jana usiku 26/10/2016. Hakuna vifo wala majeruhi kwa sababu gari lilikuwa likienda kwenye karakana ya kampuni.




Picha na : Elias M.C



Basi la kampuni ya BARCELONA linalofanya zake kati ya DAR na LINDI, Limepata ajali Eneo la MITEJO LINDI na kusababisha vifo vya watu wanne (4) na majeruhi (18). Ajali hii imetokea tarehe 17/10/2016

Chanzo cha ajali bado hakijajulikana tutaendelea kuwajuza kadri tutakavyukuwa tunapata habari.








 Picha : TBB Facebook









 Basi la kampuni ya Super Shem linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Mwanza Leo Tarehe 21/9/2016 Majira ya Asubuhi ,Likiwa linatokea Mbeya Limepata ajali katika kijiji cha Hungumalwa Mwanza,

Ajali hio imehusisha basi la Super Shem na Gari ndogo ya Abiria Hiace na kusababisha vifo na majeruhi katika gari ndogo , 

Haijathibiktika waliofariki ni wangapi mpaka sasa tutaendelea kuwajuza kadri tunavyopata taarifa.


**Vyanzo mbalimbali vya habari vinasema ajali hii imegharimu maisha ya Watu 13.




 Picha na TBB whatsapp
_________________________________________________________________________________
Basi la kampuni ya New Force namba T 429 DEU, Linalofanya safari zake kati ya Dar na Songea, Tarehe 19/9/2016 usiku majira ya Saa Mbili lilipata ajali maeneo ya kibena Mkoani Njombe

Hadi Taarifa zinatufikia ajali imesababisha vifo vya watu 12, wanawake 8 na wanaume 4, Huku ikiacha majeruhi zaidi ya 10.

Bado tunaendelea kufuatilia chanzo cha ajali tutawajuza kadri tutakavyokuwa tukipata taarifa.










Picha Credit : Whatsapp TBB

__________________________________________________________________________________
basi la kampuni ya JM luxury linalofanya kazi zake kati ya Dar na Musoma (Kanda ya ziwa), Jana alfajiri tarehe 11/9/2011, Lilipata ajali njee kidogo ya mji wa shinyanga Kolandoto.

Ajali ikiacha vifo na majeruhi,




Picha na : TBB Facebook





Basi la kampuni ya HOOD LTD , Aina ya Marcopolo Torino linalofanya kazi ruti ya Mbeya - Arusha via Chalinze limepata ajali leo 05/09/2016 eneo la Mabungo , Himo(Moshi)

Chanzo cha ajali ni mpanda pikipiki aliekatisha ghafla kuingia kituo cha mafuta na kusababisha basi kumgonga mwendesha pikipiki na basi kuanguaka 
Mpaka habari zinatufikia aliefariki ni mmoja (Mwendesha pikipiki) na mjeruhi wanne waliokuwa kwenye basi  






Picha na : Elias M. C na M Temba 

________________________________________________________________________________
Basi la kampuni ya Hai Express(Lililonunuliwa na Maguchi Exp) Limepata ajali maeneo ya Berega Mkoani Morogoro, lilipokuwa likikwepa ajali ya uso kwa uso na Star bus la Dar Mwanza

Ajali imetokea jana saa nne Usiku.  





Picha na TBB Whatsapp




Basi ya kampuni Al saedy, limechochora jana maeneo ya Msolwa Chalinze kwenye za kukwepa ajali ya uso kwa uso




Picha : Mike Temba TBB
__________________________________________________________________________________

Basi la Kampuni ya Malamsha linalofanya kazi zake kati ya Mafinga  na Ibwanzi (iringa)
 limechomwa moto na watu wasiojulikana , Hamna vifo ila majeruhi ni dada mmoja alieumia mguu katika harakati a kukimbia tukio, Wachomaji walishusha abiria kabla ya kuchoma basi.

Tukio limetokea mufindi mpakani mwa Ihanu na Kilosa


 Picha : Primogeniture TBB

_________________________________________________________________________________

Basi la kampuni ya HOKKAS linalofanya safari kati ya Simiyu na Meatu, Limepata ajali jana Tarehe 30/8/2016. 

Hakuna vifo ni majeraha tu , kwa abiria. 




Picha na: TBB Whatsapp

__________________________________________________________________________________


Basi la Kampuni ya Dar lux, linalofanya safari zake kati ya Dar na Tunduma jana Tarehe 29/8/2016 limepata ajali, Maeneo ya Iwambi Mbeya, lilipokuwa linasafiri kutoka Dar - kuelekea Tunduma.

mtoa Habari kutoka eneo la tukio anasema hakuna madhara kwa binadamu.
tutaendelea kuwajuza kadri tunavyopata habari..

POLENI TIMU DAR BLUE.

Picha na : Alekesi TBB






______________________________________________________________________________________________________


No comments:

Post a Comment